pmbet

Ancelotti ndiye kocha mwenye mafanikio zaidi Real Madrid - Luis Figo

Eric Buyanza

April 24, 2025
Share :

Nyota wa zamani wa Real Madrid, Luis Figo amemtaja meneja wa sasa Carlo Ancelotti kuwa ndiye kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya klabu hiyo.

Figo alitoa kauli hiyo alipokuwa akimtetea Ancelotti kufuatia timu yake kuondolewa kwenye UEFA Champions League na Arsenal.

"Ninajua ulimwengu huu una kumbukumbu fupi. Ni vigumu kuona zaidi ya mchezo wa hivi majuzi"

"Nilichokiona cha kushangaza ni kwamba huko Madrid kila mtu sasa hivi anatilia shaka kuhusu uwezo wa Ancelotti, ambaye ndiye kocha mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Real Madrid.

“Wengine wakiweka mijadala kujadili kama kocha huyo anafaa kuendelea kuwa meneja wa klabu hiyo au la? Mimi naona ni upuuzi, eti baada ya ile mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Arsenal, swali pekee lililoulizwa sana kwenye redio na TV lilikuwa kuhusu mustakabali wa kocha huyo. Katika soka, huwezi kushinda kila wakati," Figo aliiambia Gazzetta.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet