Andre Stander polisi mhalifu hatari kuwahi kutokea South Africa
Eric Buyanza
March 24, 2026
Share :

#JeWajua Andre Stander alikuwa afisa wa polisi nchini Afrika Kusini, lakini kwa siri kubwa alikuwa mhalifu hatari wa kuiba kwenye mabenki.
Mara nyingi alikuwa akiiba benki wakati wa mapumziko yake ya chakula cha mchana na baadaye kurudi kuchunguza uhalifu huohuo alioufanya kama sehemu ya majukumu yake ya kazi.
Baada ya kuiba karibu benki 30, Andre Stander alikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha miaka 75 jela tarehe 6 Mei 1980.
Alitoroka gerezani na baadaye akaanzisha genge la uhalifu, hatimaye aliuawa katika majibizano ya risasi na polisi mwaka 1984.





