Anelka awaweka Lamine Yamal na Mbappe kwenye mzani mmoija
Eric Buyanza
March 7, 2026
Share :

Nyota wa zamani wa Real Madrid na Arsenal, Nicolas Anelka, amemsifu kiungo wa Barcelona, Lamine Yamal, kuwa miongoni mwa wachezaji bora duniani sambamba na Kylian Mbappe.
Yamal ambaye ana miaka 18 tu, amekuwa mchezaji muhimu kwa Barcelona, akicheza mechi 78 na kufunga mabao 16 katika La Liga.
Pia ameshiriki katika mechi 23 za timu ya taifa ya Hispania, akifunga mabao 6.
"Ni mchezaji mzuri mwenye kipaji. Pia ni mdogo mmoja wa wachezaji wenye ujuzi mkubwa. Anafunga mabao na kutoa pasi za mabao. Daima anatengeneza kitu uwanjani,” Hakuna wachezaji wengi kama yeye. Hawapo tena. Tulikuwa na wachezaji wengi kama hao. Lakini sasa yeye ni mmoja wa wachezaji wenye vipaji vikubwa barani Ulaya na duniani,” alisema Anelka.
Mbappe, kwa upande mwingine, amefunga mabao 59 katika mechi 71 za Real Madrid, na mabao 256 katika mechi 308 za PSG. Anelka anaamini kuwa Yamal na Mbappe ni wachezaji wa kiwango cha juu na anawatabiria makubwa katika siku za baadae.





