ANFIELD KWALIPUKA! Liverpool yashusha mashine ya Bilioni 440
Eric Buyanza
August 31, 2026
Share :

Liverpool imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Ufaransa, Bradley Barcola, kutoka Paris St-Germain kwa ada inayoweza kufikia pauni milioni 123 (sawa na shilingi Bilioni 440.88 za kitanzania).
Awali, PSG ilimthamini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kwa pauni milioni 145, lakini Liverpool italipa kiasi cha awali cha pauni milioni 106 pamoja na pauni milioni 17 za nyongeza kulingana na vigezo fulani.
Barcola ametia saini mkataba wa miaka mitano na kuwa mchezaji wa tano mpya kujiunga na Anfield msimu huu wa joto, akifuatia usajili wa winga Victor Munoz na mabeki Jeremy Jacquet, Ronald Araujo na Ifeanyi Ndukwe.
"Ilichukua muda mrefu lakini nina furaha sana leo kuweza kuichezea Liverpool; ninachotaka tu ni kuwa uwanjani na kucheza," alisema Barcola.
"Natumai kuifikisha klabu kwenye mambo makubwa sana. Kwanza kabisa, kushinda Ligi Kuu ya Uingereza (Premier League) - hiyo ni moja ya ndoto zangu kubwa maishani.
"Lengo ni kufanya hivyo na kubaki katika timu hii kwa muda mrefu - ndiyo maana nimesaini mkataba wa muda mrefu - na natumai nitaweza kufanikisha hilo."
Barcola, ambaye atavaa jezi namba 29 huko Anfield, anapendelea kucheza winga ya kushoto lakini anaweza kucheza nafasi yoyote katika safu ya ushambuliaji.





