pmbet

'Angusha' ya Hennesseyy, yapata mapokeo mazuri

Eric Buyanza

March 13, 2024
Share :

Muigizaji na Rapa Hennesseyy ameendeleza ubabe kwenye muziki baada ya ngoma yake mpya  'Angusha' aliyomshirikisha Elly Da Bway kupata mapokeo mazuri.
 

Hennesseyy ambaye ni bosi wa lebo ya muziki ya 'Spacious Music' na kampuni ya utengenezaji filamu ya 'Spacious Films', amejizolea umaarufu kutokana aina ya video zake ambazo zimekuwa zikilenga maisha ya ulaji wa bata anayoishi.
 

Kwa mujibu wa Hennesseyy, video ya ngoma 'Angusha' ni miongoni mwa kazi alizotumia mkwanja mrefu katika utengenezaji wake.

"Maisha ya bata ndio maisha yetu halisi kwahiyo tunachokionyesha kwenye video ndio kile tunachoishi kama Spacious Music, nashukuru mapokeo ya 'Angusha' yamekuwa mazuri kwasababu tumeendelea kukaza kwa kutoa video za gharama na muziki mzuri kama kawaida yetu," alijigamba msanii huyo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet