Anthony Joshua atanua na Helikopta nchini Oman
Eric Buyanza
February 17, 2026
Share :
Bondia Anthony Joshua alisafiri katika eneo kubwa la Oman akiwa na helikopta siku ya jana (Jumatatu) akiwa mapumziko kufuatia mwanzo mbaya wa mwaka.
Joshua, mwenye umri wa miaka 36, alihusika katika ajali mbaya ya gari wakati wa safari yake kwenda Nigeria mwishoni mwa Desemba, na kuwaua marafiki zake wawili Sina Ghami na Latif 'Latz' Ayodele.
Joshua aliposti picha zake akichungulia mlango wazi wa helikopta wakati wa safari yake ya Mashariki ya Kati.
Alipiga picha akiwa ametazama kamera kwa vidole viwili huku video ikimwonyesha akiangalia jangwa la Oman pembeni kukiwa na helikopta nyingine.
AJ hivi karibuni amewekeza katika taifa hilo la Mashariki ya Kati, akinunua nyumba ya kifahari ya pauni milioni 1.2 kabla ya pambano lake tata dhidi ya Jake Paul.






