Antony Joshua amtandika Francis kwa K.O raundi ya pili
Eric Buyanza
March 9, 2024
Share :
Bingwa wa zamani wa uzito wa juu, Anthony Joshua amefanikiwa kumtandika kwa Knock Out (K.O) Francis Ngannou katika pambano la Uzito wa Juu lililofanyika Riyadh, Saudi Arabia alfajiri ya leo.
Joshua alimwangusha Ngannou katika raundi ya kwanza ya mchezo na baadaye dakika ya 2:38 ya raundi ya pili alimwangusha tena kwa ngumi nzito ya mkono wa kulia, hatua iliyosababisha mwamuzi kumaliza mchezo.