Anusurika kifo kimuujiza baada ya mkufu aliouvaa kusimamisha risasi
Eric Buyanza
June 13, 2024
Share :
Jamaa mmoja huko Colorado nchini Marekani tunaweza kusema ni mwenye bahati ya ajabu kuwa hai hadi leo hii, baada ya kunusurika kwa risasi iliyozuiliwa na mkufu wa silver aliokuwa ameuvaa shingoni.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, kulitokea ugomvi na majibishano eneo alilokuwepo jamaa huyo na ghafla ikapigwa risasi ambayo iligonga mkufu uliopunguza nguvu ya risasi hiyo na hivyo kusababisha jeraha dogo tu shingoni kwake. Polisi waliliita tukio hilo la maajabu makubwa.
Mshukiwa aliyepiga risasi hiyo alikamatwa eneo la tukio na kufunguliwa mashtaka ya kujaribu kuua.
Wiki iliyopita, Idara ya Polisi ya Jiji la Colorado ilichapisha picha za mkufu huo uliokuwa na damu kwenye ukurasa wake wa Facebook.