Anusurika kufa baada ya kumeza funguo wake wa gari
Eric Buyanza
February 2, 2024
Share :
Mwanaume mmoja nchini Saudi Arabia alilazimika kufanyiwa upasuaji wa laparoscopic ili kufungua njia yake ya hewa baada ya kumeza ufunguo wa gari lake kwa bahati mbaya alipokuwa akiuchezea mdomoni.
Kwa mujibu wa Gulf News, mwanaume huyo mwenye wa miaka 49 alilazwa katika chumba cha dharura cha hospitali huku wahudumu wakipambana kuhakikisha wanaokoa maisha yake.
Kwa bahati nzuri zoezi la upasuaji huo ulifanikiwa kwa ufunguo huo kutolewa na mgonjwa aliruhusiwa baada ya siku chache kutokana na hali yake kuendelea vizuri.