pmbet

Apandishwa kizimbani kwa kukata mtu sikio

Eric Buyanza

January 4, 2024
Share :

Mfanyabiashara Kalumna George (18) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo ya Kariakoo akikabiliwa na mashtaka ya kumjeruhi mtu kwa kumkata sikio la kushoto.
 

George alifikishwa mahakamani hapo jana mbele ya Hakimu, Gladness Njau kisha kusomewa mashtaka na karani wa mahakama hiyo, Caroline Nyonyi.
 

Nyonyi alidai kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Januari Mosi, mwaka huu, katika eneo la Upanga Sea view barabara ya Obama katika Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.
 

Alidai mshtakiwa kwa makusudi alimjeruhi kwa kumkata na kisu sikio la kushoto, Yazidu Jafari na kumsababishia maumivu mwilini jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
 

Baada ya kusomewa mashtaka hayo mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo, hivyo alirudishwa mahabusu hadi leo kwa ajili ya kesi yake kutajwa.
TSN

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet