pmbet

Apiga magoti masaa 21 kuomba msamaha kwa demu ili warudiane!

Eric Buyanza

February 1, 2024
Share :

Kijana mmoja kutoka Sichuan nchini China ametumia takriban masaa 21 akiwa amepiga magoti nje ya ofisi za mpenzi wake wa zamani kama ishara ya kuomba msamaha ili warudiane.
 

Kitendo hicho kilichowakera wanaume wengi waliokuwa wakipita eneo hilo, kilizua gumzo kwenye mitandao ya kijamii ambapo inaelezwa jamaa huyo alifika nje ya ofisi hiyo akiwa na shada la ua waridi jekundu saa 1 jioni na akabaki amepiga magoti hadi kesho yake, akistahimili mvua, baridi na macho ya wapita njia ambao wengi wao walikuwa wakimcheka na kumpiga picha.
 

Kwa kumuonea huruma baadhi ya watu iliwabidi waite polisi lakini hawakufanikiwa kumtoa. Na alisikika akihoji....“Kwani ni haramu kwangu kupiga magoti hapa? kama si haramu, tafadhali mniache,” mwanamume huyo alisema wakati polisi walipojaribu kumtaka ainuke.
 

Baadae mwanamume huyo baada ya kuona jambo lake limeshindwa kufanikiwa alionekana akichukua maua yake na kuondoka, labda kwa sababu hakuweza kuvumilia tena baridi lililokuwa likimchapa.
 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet