pmbet

Apigwa faini kwa kuruhusu wageni kula hadharani Zanzibar

Eric Buyanza

March 29, 2024
Share :

Kamisheni ya Utalii Zanzibar imethibitisha kuipiga faini ya dola 500 kampuni ya utalii ya Organisateur Francophone Tours and Travel kwa kuruhusu watalii kula hadharani katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.
 

Katika taarifa kwa umma Afisa Uhusiano wa Tume ya Utalii Zanzibar Mohamed Nassor Bajuni alisema kampuni hiyo ilikiuka miongozo na maagizo yaliyotolewa kwa wafanyabiashara wa utalii wakati huu wa mfungo wa Ramadhani.
 

"Toka kuanzishwa kwa kamisheni huo tunatoa notisi maalumu kwa kipindi cha mwezi wa Ramadhani kuhusiana na suala hili" alisema Bw.Mohamed.
 

Muongoza watalii wa kampuni hiyo, Khamis M. Kahogo pia amezuiliwa kufanya shughuli zozote za utalii kwa muda wa miezi mitatu," aliongeza kusema.
 

Kamisheni hiyo imesisitiza umuhimu wa kufuata desturi na mila za visiwa vya Zanzibar hasa wakati huu wa mfungo wa Ramadhan.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet