pmbet

Apple yawaonya wateja wa iphone kutoziweka kwenye mchele

Eric Buyanza

February 22, 2024
Share :

Kampuni ya Apple Inc. inayojishughulisha na utengenezaji simu za iPhone, imewatahadahrisha watumiaji wa simu za iPhone, kuacha kuweka simu zao kwenye mchele pale inapotokea wametumbukiza kwenye maji.
 

Apple wametoa tahadhari hiyo, kupitia tovuti yao, ambapo wamebainisha kuwa kuweka simu hizo kwenye mchele inaweza kusababisha chembechembe ndogo za nafaka hiyo, kuharibu vifaa hivyo.
 

Endapo ikitokea vifaa hivyo vimeingiliwa na maji, Kampuni hiyo imewashauri wateja wake kuchomoa waya kwenye kiunganishi (port), baada ya hapo uelekeze chini kiunganishi hicho, kisha uiweke katika sehemu kavu yenye hewa safi ikauke.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet