APR wamtaka Aziz Ki, Yanga yawatajia bei Mbaya
Sisti Herman
April 11, 2024
Share :
Kwa mujibu wa mwandishi wa habari za michezo ambaye huandika zaidi habari za uhamisho wa wachezaji, Mick Jr raia wa Ghana ameweka wazi kuwa wiki iliyopita klabu ya APR ya nchini Rwanda iliulizia uwezekano wa kumnyakua kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephanie Aziz Ki na wakaulizia bei yake sokoni.
Micky anaeleza kuwa APR walijibiwa na klabu ya Yanga kuwa thamani ya Aziz Ki kwenye soko la usajili ni dola za kimarekani milini moja (sawa na zaidi ya Bilioni 2 na nusu za Tanzania).
Ikumbukwe kuwa Aziz Ki yupo ukingoni kumaliza mkataba wake Jangwani huku vilabu mbalimbali vikubwa Afrika kama Orlando Pirates, Kaizer Chiefs na Mamelodi Sundwons vikimuwania kutokana na kiwango alichoonyesha kwenye ligi ya mabingwa Afrika hadi sasa.