APR wasusa Mapinduzi kisa waamuzi
Sisti Herman
January 10, 2024
Share :
Baada ya kutolewa kwenye mashindano ya Mapinduzi Cup 2024 katika hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penalti 4-2 dhidi ya Mlandege Kocha msaidizi wa timu ya APR, Aime Ndizeye ameonyesha kusikitishwa kwake na maamuzi ya waamuzi wa mchezo huo
Kocha huyo kwenye mkutano na waandishi wa habari alitoa kauli nzito sana kwa kukiri kuwa ni ngumu kwa timu hiyo kushiriki tena Mapinduzi Cup miaka ijayo
“Nafikiri wote mliona mchezo, kwanza tunawabeza waamuzi walikuwa upande mmoja zaidi na kwa kifupi kiukweli ni aibu kwa Zanzibar na nafikiri huu ni mwanzo wa sisi kutorudi kushiriki mashindano haya tena” alisema kocha huyo akisikitika