Arajiga akabidhiwa Yanga na Simba
Sisti Herman
April 19, 2024
Share :
Bodi ya Ligi Kuu nchini imemtangaza, Ahmed Arajiga kuwa ndiye mwamuzi wa kati katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati Yanga SC dhidi ya Simba SC.
Arajiga atasaidiwa na Mohamed Mkono kutoka Tanga, Kassim Mpanga wa Dar es Salaam huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Tatu Malogo.
Mchezo huo maarufu kama Derby ya Kariakoo itachezwa Jumamosi Aprili 20, 2024 saa 11:00 jioni katika Dimba la Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.