Arajiga apewa Simba na Azam kwa mkapa leo
Sisti Herman
February 24, 2025
Share :
Kuekelea mchezo wa Mzizima derby kati ya Simba SC dhidi ya Azam FC Uwanja wa Mkapa Leo Februari 24, Mwamuzi wa kati kutoka Mkoani Manyara Ahmed Arajiga ametangazwa kusimamia sheria 17 za soka katika mchezo huo kuanzia majira ya Saa Moja kamili usiku.
Arajiga atashirikiana na Mwamuzi msaidizi namba moja Mohamed Mkono kutoka Tanga pamoja na Kassim Mpanga kutoka Dar Es Salaam.