pmbet

Arajiga ateuliwa na FIFA

Joyce Shedrack

May 14, 2024
Share :

Ahmed Arajiga, mwamuzi kutoka Tanzania ameteuliwa na FIFA kuchezesha mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia, kati ya Malawi na São Tomé, utakaochezwa Juni 6, 2024, jijini Lilongwe nchini Malawi.

Mwamuzi huyo wa kimataifa atasaidiwa na waamuzi wengine kutoka Tanzania ambao ni Frank Komba, Kassim Mpanga na Hery Sasii.

Itakumbukwa kuwa, Arajiga ndiye aliyesimama katikati kwenye mechi mbili za watani wa jadi nchini Tanzania, Simba na Yanga, ambazo zote zilimalizika kwa ushindi kwa Yanga.

 

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet