Arajiga, Kayoko kusimamia dabi ya Kariakoo kesho
Sisti Herman
September 15, 2025
Share :
Kuelekea mchezo wa Ngao ya jamii kesho kati ya Yanga dhidi ya Simba, shirikisho la soka nchini, TFF wenye dhamana ya mchezo huo wametoa orodha ya timu ya waamuzi watakosimamia mchezo huo inayoongozwa na mwamuzi wa kimataifa wa Tanzania kwasasa Ahmed Arajiga.
Hii ni orodha rasmi ya wasimamizi wa mchezo huo;
Mwamuzi wa kati: Ahmed Arajiga
Mwamuzi msaidizi wa 1: Mohammed Mkono
Mwamuzi msaidizi wa 2: Kassim Mpanga
Mwamuzi msaidizi wa akiba: Ramadhan Kayoko
Mtathimini waamuzi: Sudi Abdi