Arbeloa aweka rekodi Real Madrid
Eric Buyanza
February 18, 2026
Share :

Kocha wa Real Madrid, Álvaro Arbeloa, amefanikisha rekodi mpya baada ya timu yake kushinda mchezo wa kwanza wa hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Benfica.
Kwa mujibu wa OptaJose, Real Madrid imeshinda mechi zake 9 zilizopita chini ya Arbeloa, na kufunga jumla ya magoli 23.
Rekodi hii ya Arbeloa ni bora zaidi tangu kipindi cha kocha Manuel Pellegrini msimu wa 2009/10, ambaye alishinda katika mechi zake 10 za kwanza.





