pmbet

Arda Guler afunga goli la Puskas, Madrid ikishinda

Sisti Herman

March 15, 2026
Share :

 

Nyota wa Real Madrid, Arda Güler, amewaacha mashabiki vinywa wazi baada ya kufunga goli la kustaajabisha kutokea umbali wa mita 72 dhidi ya Elche.

Shuti hilo la ajabu lililopigwa kutoka mbali liliipa goli la mwisho katika ushindi mnono wa mabao 4–1 dhidi ya Elche.

Goli hilo, lililopigwa kwa usahihi mkubwa kutokea upande wake wa uwanja, limezua mjadala mzito ulimwenguni kote, huku wachambuzi wengi wakidai kuwa linastahili kushinda Tuzo ya Puskas.

Halikuwa goli la kawaida; lilikuwa ni dhihirisho la kipaji cha hali ya juu duniani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet