Argentina chupuchupu Copa-America, Messi akosa penati
Sisti Herman
July 5, 2024
Share :
Huu ni mkwaju wa penati aliyokosa nahodha wa timu ya Taifa Argentina Lionel Messi elo alfajiri kwenye mchezo wa robo fainali ya kombe la mataifa Ulaya (Copa-America) dhidi ya Ecuador, Argentina wakipita wa penati.
Mchezo huo uliochezwa kwa dakika 120 na kushuhudia sare ya 1-1 uliamuliwa kwa mikwaju ya penati ambapo Argentina walishinda penati 4-2 huku Messi akikosa penati ya kwanza.
Baada ya ushindi huo Argentina wamefuzu hatua ya nusu fainali na watacheza na mshindi kati ya Canada na Venezuela.