Argentina kustaafisha jezi ya Messi
Sisti Herman
December 31, 2023
Share :
Shirikisho la soka nchini Argentina linapanga kustaafisha jezi namba 10 inayotumiwa na mshambuliaji na nahodha wa timu ya Taifa na klabu ya Inter Miami ya ligi kuu nchini Marekani, Lionel Messi pale ambapo mshambuliaji huyo mshindi wa Ballon D'or mara 7 atakapostaafu kuchezea timu hiyo ya Taifa.
Hata hivyo uamuzi huo unaonekana kupata ukinzani mkubwa kutoka kwa mashabiki na wadau wa soka huku wengi wakidai walipaswa kustaafisha wakati Diego Maradona, gwiji wa soka nchini humo anastaafu.