pmbet

Argentina yaitandika Colombia na kutwaa taji la 16 la Copa America

Eric Buyanza

July 15, 2024
Share :

Argentina imeunyakua ubingwa wa Copa America kwa kuitandika Colombia kwa bao 1-0, katika mchezo wa Fainali uliofanyika alfajiri ya leo katika Uwanja wa Hard Rock nchini Marekani.

Bao la Lautaro Javier Martínez limeipa Argentina ubingwa mara ya pili mfululizo na kuingia kwenye rekodi ya kulichukua kombe hilo kwa mara ya 16.

Haikuwa kazi rajhisi kwa Argentina kwani iliwalazimu kucheza kwa dakika 120, baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana hadi dakika 90.

Dakika ya 112 mashabiki wa Argentina waliamshwa kwa furaha iliyodumu hadi mwisho wa mchezo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet