Argentina yapata pigo kuwakosa watatu dhidi ya Brazil na Uruguay.
Joyce Shedrack
March 20, 2025
Share :
Timu ya Taifa ya Argentina itawakosa wachezaji wake 3 muhimu Lionel Messi,Lautaro Martínez na Paulo Dybala katika mechi 2 zijazo za kufuzu kombe la Dunia dhidi ya Brazil na Uruguay kutokana na majeraha yanayowasumbua nyota hao.

Messi na Martinez wanasumbuliwa na majeraha ya misuli wakiwa na matumaini ya kurejea uwanjani hivi karibuni wakati Paulo Dybala akikosekana mpaka mwishoni mwa mimu huu kutokana na jeraha kubwa la misuli linalomsumbua huku akitarajia kufanyiwa upasuaji hivi karibuni.
Argentina itashuka dimbani jumamosi hii ya tarehe 22 march kukipiga na Uruguay kabla ya wiki ijayo tarehe 26 march kucheza na Timu ya Taifa ya Brazil.