Arne Slot akanusha kuondoka Liverpool
Sisti Herman
May 14, 2026
Share :

Kocha mkuu wa Liverpool, Arne Slot amethibitisha kuwa hatoondoka Liverpool mwishoni mwa msimu huu, atabaki kwenye timu hiyo licha ya kuwa na msimu usioridhisha.
"Mazungumzo yamekuwa yakiendelea kati ya klabu na wachezaji wapya, na mimi nahusika katika hilo. Nina kila sababu ya kuamini mimi ni meneja wa Liverpool msimu ujao", Slot amethibitisha hivi punde.
"Kwanza kabisa, nina mkataba na klabu hii, na pili, kutoka kwa mazungumzo yote tunayofanya. Hiyo ni maoni yangu juu yake na ni wazi sana".





