pmbet

Arne Slot kuhamia jumba la kifahari analoishi Jurgen Klopp

Eric Buyanza

May 11, 2024
Share :

Kocha wa kiholanzi Arne Slot anatazamiwa kuchukua mikoba ya Jürgen Klopp kama meneja wa Liverpool mwishoni mwa msimu huu na kuhamia kwenye jumba la kifahari analoishi Jurgen Klopp lenye thamani ya dola milioni 5.

Magari ya kubebea mizigo yameonekana nje ya jumba hilo la kifahari lenye vyumba saba vya kulala, ikiwa ni ishara ya kuonyesha kwamba Klopp ameanza kufangasha mizigo kidogo kidogo.

Baadhi ya vilivyomo kwenye jumba hilo ni vyumba vitatu vya mapumziko, chumba cha kuangalizia filamu, bwawa la kuogelea la ndani na bustani kali sana kupita maelezo.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet