Arsenal, Barca mzigoni leo UEFA
Sisti Herman
March 12, 2024
Share :
Ligi ya mabingwa Ulaya hatua ya robo fainali mkondo wa pili unaendelea leo ambapo Barcelona na Arsenal zitatakiwa kufanya kazi kubwa ili kuhakikisha zinatinga hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Arsenal ambayo ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Porto kwenye mchezo wa kwanza ugenini, leo itakuwa nyumbani kuhakikisha inapindua matokeo hayo ili iweze kufuzu kwenye hatua hiyo muhimu.
Kwa upande wa Barcelona ambayo ilionyesha kiwango cha juu kwenye mchezo wa kwanza ugenini na kutoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Napoli, leo inarejea nyumbani kuhakikisha inapata ushindi na kufuzu.
Mabingwa watetezi wa michuano hiyo mikubwa Ulaya Manchester City pamoja na mabingwa wa kihistoria Real Madrid tayari zimeshafuzu sawa na Bayern Munich na Paris Saint-Germain.
Timu zote zinazocheza leo na kesho zina nafasi ya kufuzu kutokana na matokeo ya michezo ya mkondo wa kwanza kwa kuwa hakuna iliyopoteza kwa zaidi ya bao moja.
Matokeo mechi tano za nyuma Arsenal vs Porto:
Arsenal 4-0 Porto
Porto 2-0 Arsenal
Porto 2-1 Arsenal
Arsenal 4-0 Porto
Porto 1-0 Arsenal.
Mechi tano za Barcelona vs Napoli
Napoli 1 – 1 FC Barcelona
Napoli 2 – 4 FC Barcelona
FC Barcelona 1 - 1Napoli
FC Barcelona 3 – 1 Napoli
Napoli 1 – 1 FC Barcelona.