Arsenal Defensive Principles under Mikel Arteta
Sisti Herman
June 12, 2024
Share :
Kwenye ligi kuu Uingereza msimu wa 23/24, Arsenal ndiyo timu bora zaidi kiuzuiaji, ikiwa na takwimu bora kuliko timu nyingine yoyote;
- Mechi 38
- Magoli ya kufungwa 29
👉 Mara baada ya mchezo kati ya City dhidi ya Arsenal, City walikuwa na takwimu hizi;
- Ball Possession 73%
- Pass 700+
👉 City walikua na wastani mzuri sana kuwa na mpira Ila hawakutengeneza madhara kwenye lango la Arsenal
- Chances created 2
- Shot on target 1
- Expected Goals (1.02)
👉 Hii ina maana City walitawala na mpira bila madhara huku Arsenal wakitawala uzuiaji kwa kishikilia bomba vizuri kwasababu ya mbinu zao za uzuiaji.
Mikel Arteta ameisuka vyema sana timu yake kimbinu kwenye Moments isipokuwa na umiliki wa mpira
👉 Arsenal wakizuia kwenye theluthi zao mbili za nyuma (Mid & Low Block )huzuia na mfumo wa 4-4-2, ambapo mistari ya uzuiaji huwa;
- 1st line: Kai na Odergaard
- 2nd line: Saka & Gabriel (Martinelli/Jesus) pembeni na Rice & Jorginho kati
- 3rd line: Ben White & Kiwior pembeni na Gabriel & Saliba Kati
👉 Muundo huu umewapa balance kuzuia njia za kati na pembeni za wapinzani wao, ambapo;
- Kai na Odergaard huzuia build up za wapinzani kupita Kwa njia za kati kwa kuvunja mawasiliano Kati wanaojenga shambulizi na wanaoendeleza shambulizi (Build up Phase)
- Rice na Jorginho huzuia viungo wa kati wanaoweza kupokea na kuendeleza build up Katikati ya mistari (build up progressions)
- Saka na Gabriel huzuia full backs wa wapinzani kuendeleza shambulizi kwa njia za pembeni, pia hu-track mikimbio yao ili wasitengeneze wide Overloads, yaani Full-backs wao Ben White & (Kiwior, Tomiyasu, Zinchenko) wasizidiwe idadi na Full-backs na Wingers wa wapinzani
- Wapinzani wakipita juu, Saliba na Gabriel wapo gado kushinda kila situation
👉 Sifa za mbinu za Arsenal kwenye muundo wao wa uzuiaji ni Kama;
- Recovery runs Bora - wachezaji wao kurudi kwa haraka kwenye shape pindi wasipokuwa na mpira
- Compactness - kudumisha muundo wakiwa pamoja Bila gapes kubwa
- Winning duels - Wachezaji wa Arsenal wapo Committed sana kushinda kila situation za kugombania mipira
- David Raya as Sweeper