pmbet

Arsenal inaangalia uwezekano wa kumsajili Vinicius Jr.

Eric Buyanza

July 27, 2026
Share :

Arsenal wana nia dhati ya kumsajili Vinicius Junior kutoka Real Madrid na wako tayari kumfanya kuwa mchezaji wao anayelipwa mshahara mkubwa zaidi kuwahi kutokea.

 

Kwa mujibu wa gazeti la UK Telegraph, Arsenal wako tayari kumpa mchezaji huyo mshahara wa kushangaza ili kumshawishi, kwa sasa analipwa pauni 400,000 kwa wiki.
Mchezaji anayelipwa mshahara wa juu zaidi Arsenal ni Bukayo Saka. Anapokea pauni 300,000 kwa wiki.

 

Vinicius Jr ameingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake na Real Madrid. Mazungumzo ya kuongeza mkataba mpya yamegonga mwamba kwa sababu mchezaji huyo anataka mshahara mkubwa unaolingana na ule wa Kylian Mbappé. Madrid wanaweza kulazimika kumuuza dirisha hili ili wasimpoteze bure mwakani.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet