Arsenal kufanya vipimo vya jeraha la Grabiel
Joyce Shedrack
November 17, 2025
Share :
Beki wa Arsenal Gabriel Magalhaes atafanyiwa tathmini na madaktari wa Arsenal wiki hii wakitaka kujua ukubwa wa jeraha lililomlazimu kujiondoa kwenye kikosi cha timu ya soka Taifa ya Brazil.

Beki huyo aliachwa na Brazil siku ya Jumapili baada ya uchunguzi kuonyesha alikuwa na jeraha la misuli katika goti lake la kulia
Gabriel alipata jeraha Jumamosi wakati Brazil ikishinda 2-0 dhidi ya Senegal kwenye Uwanja wa Emirates.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 alichechemea zikiwa zimesalia dakika 30 tu za kucheza na hatasafiri na kikosi cha Brazil kwa mechi yao ya kirafiki dhidi ya Tunisia mjini Lille siku ya Jumanne na badala yake atafanyiwa tathmini na madaktari wa Arsenal wiki hii kabla ya mechi ya London Derby dhidi ya Tottenham, Jumapili hii.





