Arsenal kulipa pauni milioni 60 ili wampate beki wa Newcastle
Eric Buyanza
January 10, 2026
Share :
Arsenal iko kwenye harakati za kumsajili Tino Livramento anayetajwa kuwa moja ya beki bora kwenye ligi kuu ya Uingereza.
Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, klabu hiyo ya jiji la London inavutiwa mno na mchezaji huyo wa Newcastle licha ya kwamba amekuwa akifuatiliwa kwa ukaribu pia na Manchester City.
Uwezo mkubwa wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 umewavutia Arsenal, kwani ana uwezo wa kucheza upande wa kushoto na kulia wa safu ya ulinzi.
Inaelezwa kuwa Newcastle hawataki kumpoteza Livramento kiurahisi na hivyo watahitaji angalau kiasi cha pound milioni 60 kwa ajili ya beki huyo.






