Arsenal, Liverpool, Man U waambiwa waandae Euro Milioni 100 kumpata Antonio Silva
Eric Buyanza
May 23, 2024
Share :
Klabu za Arsenal, Liverpool na Manchester United wameripotiwa kufanya mazungumzo na Benfica kuhusu uwezekano wa kumnunua Antonio Silva.
Vilabu hivyo vitatu vya Premier League vinatamani kupata huduma ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kwenye dirisha kubwa la usajili.
Taarifa zinasema beki huyo mwenye umri wa miaka 20 anagharimu takriban Euro milioni 100.