Arsenal na Liverpool kwenye vita ya kumnasa Ayyoub Bouaddi
Eric Buyanza
June 15, 2026
Share :
Arsenal wameripotiwa kuanza mazungumzo ya kumsajili kiungo chipukizi wa klabu ya Lille ya Ufaransa, Ayyoub Bouaddi mwenye umri wa miaka 18, ambaye aliisaidia Morocco kupata sare ya 1-1 dhidi ya Brazil katika mchezo wao wa ufunguzi wa Kombe la Dunia 2026.
Kwa upande mwingine Liverpool nao wanaelezwa kuwa kwenye mazungumzo kama hayo na wawakilishi wa kiungo huyo ambaye anaweza kuzigharimu timu hizo kitita kisichopungua pauni milioni 60 (Bilioni 211 za kitanzania).






