pmbet

Arsenal na Man City waondolewa robo fainali Uefa

Sisti Herman

April 18, 2024
Share :

Ni rasmi sasa ligi kuu Uingereza haitakuwa na timu kwenye hatua ya nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya mara baada ya klabu kubwa mbili, Arsenal na Manchester City kuondolewa kwenye hatua ya robo fainali jana usiku.

Arsenal wameondolewa nyumbani kwenye dimba la Emirates kwa kufungwa 1-0 na Bayern Munich na kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2, walianzia ugenini kupata sare ya 2-2.

Man City wameondolewa nyumbani kwenye dimba la Etihad kwa kufungwa kwa matuta 4-3 baada ya sare ya 3-3 waliyopata ugenini na 1-1 waliyopata nyumbani jana.

Fainali za michuano hiyo zitachezwa kwenye dimba la Wembley, London Uingereza bila kushuhudia timu kutoka Uingereza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet