Arsenal na Man City zaigombea saini ya Bruno Guimaraes
Eric Buyanza
April 24, 2024
Share :
Klabu za Arsenal na Manchester City zinamenyana kumnunua kiungo wa Newcastle United, Bruno Guimaraes kwenye dirisha kubwa la usajili.
Timu hizo hii ni mara ya pili mfululizo wanakutana kwenye vita ya kugombea mchezaji baada ya msimu uliopita kujikuta kwenye vita ya kumgombea Declan Rice ambapo Arsenal alishinda vita hiyo kwa kukubali kulipa ada iliyovunja rekodi ya klabu hiyo ya pauni milioni 105 kwa West Ham United.