Arsenal na Man United kutoana roho mbio za kuwania saini ya Zirkzee
Eric Buyanza
June 12, 2024
Share :
Manchester United na Arsenal wanajiandaa kuingia kwenye vita ya kumnunua mshambuliaji wa Bologna Mholanzi Joshua Zirkzee, ambaye mkataba wake una kipengele cha kuachiliwa cha Pauni milioni 34.
Mholanzi huyo mwenye umri wa miaka 22 alifunga mabao 11 katika mechi 34 za Serie A msimu uliomalizika hivi karibuni na kusaidia Bologna kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa.
Manchester United mpaka sasa bado hawajui meneja wao atakuwa nani msimu ujao, lakini hiyo haiwazuii Mashetani hao Wekundu kushambulia soko la usajili.
Dirisha la usajili litafunguliwa rasmi Ijumaa Juni 14 na kufungwa Agosti 30.