Arsenal waitaka huduma ya mshambuliaji Brian Brobbey
Eric Buyanza
May 25, 2024
Share :
Katika kutaka kuboresha safu yao ya ushambuliaji, klabu ya Arsenal imekuwa ikiwafuatilia washambuliaji kadhaa msimu huu.
Hata hivyo mshambuliaji wa Ajax, Brian Brobbey ameonekana kuwa chaguo namba moja na la bei nafuu kwa 'The Gunners'
Brobbey amekuwa na wakati mzurii msimu huu akiwa na mabao 22 na asisti 12 kwenye mashindano yote, anaweza kuwa mchezaji bora na wa muda mrefu kwa Arsenal.