Arsenal wakamilisha usajili wa kudumu wa David Raya
Eric Buyanza
July 5, 2024
Share :
Arsenal wamekamilisha usajili wa kudumu wa mlinda mlango David Raya kutoka Brentford.
The Gunners wamelipa pauni milioni 27 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Uhispania, juu ya ada ya pauni milioni 3 waliyolipa Brentford kumchukua Raya kwa mkopo msimu uliopita.
"Baada ya mwaka mmoja kwa mkopo, hatimaye naweza kusema kwamba mimi ni mchezaji wa Arsenal kwa miaka ijayo. Ninafurahi kuona yajayo lakini ninaishi kila wakati na kufurahia. Ni ndoto kuwa hapa" amesema Raya.