Arsenal wako tayari kulipa pauni milioni 60 kumnunua Brahim Diaz
Eric Buyanza
March 16, 2024
Share :
Taarifa zinasema kwamba The Gunners wako tayari kulipa pauni milioni 60 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Brahim Diaz wakati wa dirisha kubwa la usajili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa na mchango mkubwa kwa Los Blancos msimu huu, akifunga mara nne na kutoa assist mbili za mabao katika mechi 23 za La Liga kwa klabu hiyo ya Madrid.
Arsenal waeonesha nia ya kupata huduma za mshambuliaji huyo na tayari wameshawasilisha ofa yao.
Mikel Arteta ameweka kipaumbele cha kumnasa Diaz kabla ya majira ya kiangazi.