pmbet

Arsenal wako tayari kumuuza Zinchenko

Eric Buyanza

June 4, 2024
Share :

Arsenal wako tayari kumuuza Oleksandr Zinchenko kwenye dirisha kubwa la usajili.

Vyanzo vinasema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 "hana furaha" ndani ya timu hiyo baada ya mara nyingi kuwa anaanzia benchi.

Zinchenko anatamani kuwa anaanza kwenye kikosi cha kwanza jambo ambalo kwasasa limekuwa gumu pale Emirates Stadium huku nafasi yake ikitendewa haki na Jakub Kiwior.

Arsenal walilipa ada ya awali ya pauni milioni 30 pamoja na nyongeza ya pauni milioni 2 ili kumpata mchezaji huyo wa kimataifa wa Ukraine mwaka 2022.

Beki huyo anafuatiliwa na vilabu vingi huku Bayern Munich wakihusishwa na kutaka kumnunua.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet