"Arsenal walinyimwa tuta, mwamuzi kapuyanga" Rio Ferdinand
Sisti Herman
April 10, 2024
Share :
Aliyekuwa beki wa Manchester United na tumu ya Taifa ya Uingereza Rio Ferdinand ambaye kwasasa ni mchambuzi wa soka kwenye vituo vya televisheni barani Ulaya wakati akitoa tathmini yake baada ya mchezo kati ya Arsenal na Bayern Munchi uliomalizika kwa sare ya 2-2 amesema kuwa mwamuzi wa mchezo huo amewanyima penalti ya wazi Arsenal baada ya kipa wa Bayern Manuel Neuer kumchezea madhambi winga wa Arsenal Bukayo Saka.
"Siamini kama kuwa pale mwamuzi hakutoa tuta, lile ni penati ya wazi kabisa, siamini" alisema Rio kwa kushangaa.
Mchezo huo ulimalizika kwa sare ya 2-2, magoli ya Arsenal yalifungwa na Bukayo Saka na Leandro Trossard huku yale ya Bayern yakifungwa na Serge Gnabry pamoja na mshambuliaji na nahodha wa Uingereza Harry Kane.