pmbet

Arsenal wanajipanga kumsajili nyota wa Serie A,

Eric Buyanza

January 6, 2024
Share :

Mchezaji huyo Fikayo Tomori mwenye umri wa miaka 26 amekuwa na wakati mzuri tangu amehamia AC Milan na amejidhihirisha kuwa mmoja wa mabeki bora wa kati katika soka la Italia hivi sasa. 

The Gunners tayari wameonyesha nia yao ya kutaka kumsajili mchezaji huyo, lakini inaonekana haiwezekani mchezaji huyo kuondoka mwezi huu...kwani Milan haitataka kudhoofisha kikosi chake kwasasa na jambo lolote litapaswa kusubiri hadi dirisha la usajili la kiangazi. 

Ripoti zinasema kwamba familia ya mchezaji huyo ni mashabiki wa Arsenal na hiyo inaweza kuwa faida kwa The Gunners watakapotaka kumsajili mwishoni mwa msimu huu. Tomori mwenyewe ni shabiki mkubwa wa Thierry Henry. 

Tomori alishindwa kufanya vyema alipokuwa Chelsea, na pengine atajihisi ya kwamba ana deni kubwa na waingereza.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet