Arsenal wanakaribia kuipata saini ya beki wa Bologna
Eric Buyanza
July 13, 2024
Share :
Arsenal wanakaribia kufikia makubaliano ya kumnunua beki wa Italia na klabu ya Bologna Riccardo Calafiori.
Bologna wameweka dau la pauni milioni 42 kwenye kichwa cha kinda huyo mwenye umri wa miaka 22 baada ya mchezaji huyo kuwasaidia kufuzu Ligi ya Mabingwa na kushika nafasi ya tano kwenye Ligi ya Serie A msimu uliopita.