pmbet

Arsenal waonesha nia ya kuitaka huduma ya Cristian Romero

Eric Buyanza

August 8, 2026
Share :

Arsenal wana hamu kubwa ya kumsajili Cristian Romero kutoka kwa wapinzani wao wa Kaskazini mwa jiji la London, Tottenham Hotspur.

 

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, 'Washika bunduki wa jiji la London' tayari wamezungumza na mawakala wa Romero kuhusu uwezekano wa uhamisho.

 

Spurs wanafahamu kuhusu nia ya Arsenal lakini ni wazi hawako tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kw mpinzani wao labda kama ingekuwa timu ya nje ya Uingereza.
 

Kwa sasa, Atletico Madrid ndiyo timu inayoonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kumsajili Romero.
 

Hata hivyo, inaripotiwa kuwa Inter Milan ilifikia makubaliano na Spurs kuhusu ada ya uhamisho ya pauni milioni 34, lakini haijafikia makubaliano na Romero kuhusu maslahi yake binafsi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet