Arsenal washinda dabi ya London Kaskazini
Sisti Herman
April 28, 2024
Share :
Ikiwa ni wiki moja tu tangu waibamize klabu ya Chelsea 5-0 kwenye 'London Derby' leo klabu ya Arsenal imeshinda tena dabi nyingine ya jiji la London na mara hii ni dhidi ya majirani zao wa London Kaskazini, Tottenham Hotspurs 3-2 kwenye dimba la nyumbani la Spurs.
Baada ya ushindi huo wababe hao wa London bado wameendelea kuwa na matumaini ya kuendelea kushindania ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza kwani hadi sasa wana alama 80 wakiwa wamecheza michezo 35, wakishindana na City wenye balama 79 huku wakiwa na mchezo mmoja mkononi.
Magoli ya Arsenal kwenye mchezo huo yamefungwa na Kai Havertz, Bukayo Saka na bao la kujifunga la kiungo wa Spurs Hojbjerg huku yale ya Spurs yakifungwa na H.M Son na Cristian Romero.