Arsenal yaitia adabu Chelsea, Kai hana huruma
Sisti Herman
April 24, 2024
Share :
Klabu ya Arsenal usiku wa jana imewapa majirani zao Chelsea kipigo cha 'Mbwa mwizi' baada ya kuwabamiza 5-0 kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza iliyochezwa kwenye dimba la nyumbani la Arsenal, Emerates.
Kwenye mchezo huo ambao Arsenal walichezea "Hamsa au 5G" magoli ya Arsenal yamefungwa na aliyekuwa mchezaji wa Chelsea, Kai Havertz aliyefunga mawili, Benjamin White aliyetupia mawili pia pamoja na Leandro Trossard aliyefunga moja.
Kwa matokeo hayo Arsenal inasalia kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na alama 77, mchezo mmoja mbele ya Liverpool wenye alama 74 na michezo miwili mbele ya Man City wenye alama 73 huku Chelsea wakiendelea kushikilia nafasi ya 9 na alama 47.