pmbet

Arsenal yajipanga kuvunja kibubu Januari kwa ajili ya Alex Baena

Eric Buyanza

October 23, 2026
Share :

Arsenal inaripotiwa kuweka nguvu kubwa katika mchakato wa kumsajili winga wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Hispania, Alex Baena katika dirisha la usajili la Januari linalokuja.
 

Arteta anatafuta kuongeza nguvu kwenye safu yake ya ushambuliaji ili kuendeleza mapambano ya kuwania mataji msimu huu, na uwezo wa Baena wa kucheza pembeni na hata eneo la kiungo mchezeshaji unamfanya kuwa chaguo bora.

 

Hata hivyo, uhamisho huo hautakuwa rahisi kwani Atletico Madrid wana mkataba mrefu na nyota huyo unaoenda hadi Juni 2030, na hawako tayari kumwachia kirahisi bila kupata dau kubwa la usajili.

 

Mazungumzo ya awali kati ya klabu hizo mbili tayari yameanza ili kuona uwezekano wa kufikia makubaliano kabla ya dirisha kufunguliwa rasmi.

pmbet
pmbet

Leagues standings

Tanzania Premier League
pmbet
pmbet