Arsenal yangia vitani na vigogo kuisaka saini ya Bakayoko
Eric Buyanza
June 27, 2024
Share :
Arsenal wameingia kwenye mbio za kuipata huduma ya mchezaji Johan Bakayoko katika dirisha la usajili na tayari wameshafanya nae mazungumzo ya awali.
Bakayoko anayechezea klabu ya PSV Eindhoven na timu ya taifa ya Uholanzi anakadiriwa kuwa na thamani ya Euro Milioni 55 mpaka 60.
The Gunners wanataka kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21, huku Liverpool, Chelsea na Bayern Munich pia zikionesha nia ya kumuhitaji.