Arsenal yashusha beki kutoka Italia
Sisti Herman
July 25, 2024
Share :
Klabu ya Arsenal imefanikiwa kuinasa saini ya beki wa timu ya Taifa ya Italia na klabu ya Bologna Riccardo Calafiori kwa ada ya uhamisho ya Euro milioni 50 (zaidi ya Tsh Bilioni 140) kwaajili ya kuwa mchezaji wao mpya.
Calafiori mwenye umri wa miaka 22 amekubali kumwaga wino kwa mkataba wa miaka mitano huku Bologna ikijumuisha kifungu cha kunufaika na mauzo ya nyota huyo siku za usoni.
Beki huyo anaenda kuungana na visiki wengine kama Benjamin White , William Saliba , Gabriel Magalhaes, Jurrien Timber na Takehiro Tomiyasu kwenye ukuta wao ambao umekuwa bora zaidi kuliko timu zingine msimu uliopita.